Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) ni taasisi rasmi ya Kiislamu nchini Tanzania iliyoanzishwa tarehe 16 Desemba 1968, kwa lengo la kuunganisha Waislamu wa Tanzania chini ya uongozi mmoja na kuratibu shughuli zote za Kiislamu nchini.
Kuanzishwa kwa BAKWATA kulitokana na haja ya kuwa na chombo madhubuti kitakachosimamia masuala ya dini ya Kiislamu kwa utaratibu unaoeleweka, pamoja na kuimarisha umoja, mshikamano na maendeleo ya Waislamu nchini Tanzania.
BAKWATA ina mfumo wa uongozi unaoanzia ngazi ya taifa hadi ngazi za chini ambazo ni pamoja na mikoa, wilaya, kata na misikiti.
Kwa miaka mingi tangu kuanzishwa kwake, BAKWATA imekuwa mstari wa mbele katika kukuza elimu ya Kiislamu, kuimarisha maadili mema ya jamii, kusimamia shughuli za Hajj na Umrah.
Leo hii, BAKWATA inaendelea kuwa taasisi muhimu inayochangia katika maendeleo ya jamii ya Kiislamu na Taifa kwa ujumla.
BAKWATA ni sauti ya Waislamu Tanzania. Tunafanya kazi kwa bidii kuimarisha imani, elimu, na ustawi wa jamii ya Kiislamu.
Chati ifuatayo inaonyesha mpangilio wa uongozi kuanzia Ngazi ya Wilaya hadi Ngazi ya Msikiti.
Kusimamia misikiti na kuhakikisha ibada zinafanywa ipasavyo.
Kusaidia madrasa na shule za Kiislamu kutoa elimu bora.
Kusaidia jamii kujiinua kiuchumi na kijamii.