Tunachofanya kwa Jamii

BAKWATA Wilaya ya Temeke inatoa huduma mbalimbali kwa waislam na jamii kwa ujumla

Huduma za Kisharia na Kidini

Usuluhishi wa Migogoro ya Ndoa

BAKWATA inasaidia wanandoa wanaopitia ugumu katika ndoa zao kupitia ushauri wa kisaikolojia na dini. Tunajaribu kulinda familia na kuimarisha mahusiano.

Hatua: Kufungua shauri → Khudhuria kwenye baraza → Usuluhishi

Talaka (Talaq)

Kutoa elimu na ufafanuzi juu ya talaka, na taratibu za kutoa au kupata talaka kwa mujibu wa sharia ya dini.

Muhimu: Wasiliana nasi kabla ya kuchukua hatua yoyote

Mirathi (Urithi)

Tunasaidia familia kusimamia na kugawanya mirathi kwa mujibu wa sharia za Kiislamu (Fara'id). Tunakusaidia kuelewa haki yako ya kisharia.

Huduma: Ushauri wa bure wa awali

Migogoro ya Kifamilia

Tunasaidia familia zenye ugumu wa ndani — migogoro kati ya wazazi na watoto, ndugu, au wanafamilia wengine — kupitia ushauri na upatanisho wa kindini.

Migogoro ya Misikiti

Tunasaidia kusuluhisha migogoro ndani ya misikiti — masuala ya usimamizi, uongozi, mali, au migogoro kati ya wanajamii wa msikiti.

Migogoro ya Madrasa

Tunasimamia na kusuluhisha migogoro inayotokea ndani ya madrasa — kati ya wazazi, walimu, au usimamizi — ili kuhakikisha elimu inaendelea bila usumbufu.

Migogoro ya Kijamii

Tunasaidia kusuluhisha migogoro mbalimbali ya kijamii ndani ya jamii ya Kiislamu, kwa njia ya amani na kulingana na mwongozo wa Qur'an na Sunnah.

Ndoa (Nikah)

Tunasimamia ndoa za Kiislamu kupitia wafungishaji ndoa wetu wenye leseni za BAKWATA na RITA. Tunasaidia katika utaratibu wote wa ndoa ya kisharia.

Huduma za Utawala

Barua Rasmi

Tunatoa barua rasmi za BAKWATA kwa taasisi na watu binafsi.

Vibali

Tunatolea vibali vya shughuli mbalimbali za Kiislamu wilayani.

Miongozo

Tunatoa miongozo ya kisharia na kidini kwa taasisi na jamii.

Usajili wa Taasisi

Tunasaidia usajili wa misikiti, madrasa, na taasisi za Kiislamu.

Leseni za Wachinjaji

Tunatolea leseni za uchinjaji wa halal kwa wachinjaji waliohitimu.

Leseni za Wafungishaji Ndoa

Tunatoa leseni za BAKWATA kwa wafungishaji ndoa waliohitimu.

Je, Unahitaji Huduma Yoyote?

Ofisi yetu iko wazi kwa huduma zote. Wageni wanapokelewa ofisini au unaweza kuwasiliana nasi kupitia simu na barua pepe.

Saa za Kazi: Jumatatu – Ijumaa, 8:00 AM – 5:00 PM

Wasiliana Nasi Angalia Fomu za Maombi